Exodus 38:9-20

Ua Wa Hema La Kukutania

(Kutoka 27:9-19)

9 aKisha akatengeneza ua. Upande wa kusini ulikuwa na urefu wa dhiraa mia moja,
Dhiraa 100 ni sawa na mita 45.
na ulikuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri,
10pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. 11Upande wa kaskazini ulikuwa na urefu wa dhiraa mia moja, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.

12Upande wa mwisho wa magharibi ulikuwa na upana wa dhiraa hamsini
Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5.
na ulikuwa na mapazia, na nguzo kumi na vitako vyake kumi, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.
13Upande wa mwisho wa mashariki jua linakochomoza, pia ulikuwa na upana wa dhiraa hamsini. 14Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano
Dhiraa 15 ni sawa na mita 6.75.
yalikuwa upande mmoja wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu.
15Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano yalikuwa upande mwingine wa ingilio la ua, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. 16Mapazia yote yaliyozunguka ua yalikuwa ya kitani iliyosokotwa vizuri. 17Vitako vya nguzo vilikuwa vya shaba. Kulabu na tepe juu ya nguzo zilikuwa za fedha, na ncha zake zilifunikwa kwa fedha. Kwa hiyo nguzo zote za ua zilikuwa na tepe za fedha.

18 ePazia la ingilio la ua lilikuwa la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo lilikuwa na urefu wa dhiraa ishirini kama zile za kwenye ua, na kimo chake kilikuwa dhiraa tano, 19likiwa na nguzo nne na vitako vinne vya shaba. Kulabu zake na tepe zake zilikuwa za fedha, na ncha zake zilikuwa zimefunikwa kwa fedha. 20 fVigingi vyote vya maskani na vya ua ulioizunguka vilikuwa vya shaba.

Copyright information for SwhNEN